pmbet

Maafisa utamaduni na michezo kupimwa kwa maendeleo ya sekta hizo - Ndumbaro

Eric Buyanza

June 18, 2024
Share :

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro @damasndumbaro_official amewaelekeza Maafisa Utamaduni na Michezo katika ngazi Mkoa, Halmashauri na Wilaya wasimamie urasimishaji wa kazi za sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa ukamilifu na wataanza kupimwa utekelezaji kuanzia mwezi Julai, 2024.

Mhe. Ndumbaro amesema hayo Juni 17, 2024 mkoani Tabora katika kikao maalum na maafisa hao juu ya mpango wa wizara kuanzisha mashindano ya mpira wa miguu kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 yatakayojulikana kama “Mwalimu Nyerere Liberation Cup” na Tamasha la Sanaa “Mwalimu Nyerere Liberation Arts Festival” kwa lengo la kuenzi mchango wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika ukombozi wa nchi za Bara la Afrika.

“Kuanzia Julai 1, 2024 katika urasimishaji wa kazi za Utamaduni, Sanaa na Michezo tutaanza kuwapima katika utekekezaji wa jambo hilo, tutatoa zawadi kwa atakaye fanya vizuri kuanzia wa kwanza hadi wa tatu” amesema Mhe. Ndumbaro.

Katika hatua nyingine Mhe. Ndumbaro amewataka maafisa hao watumie fursa ya mashindano hayo yatakayoanzishwa kuibua na kukuza vipaji katika maeneo yao. @urithiwaukombozi @chamusta_tanzania @suleiman_serera

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet