pmbet

Maajabu: Jiwe la kilo 3 latolewa kwenye kibofu cha mgonjwa

Eric Buyanza

August 20, 2026
Share :

Madaktari wa Hospitali Kuu ya Wilaya ya Trincomalee nchini Sri Lanka wamefanikiwa kufanya upasuaji wa kihistoria na kuondoa jiwe lenye uzito wa kilo 3.1 kutoka kwenye kibofu cha mkojo cha mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 55


Mgonjwa huyo alilazwa hospitalini baada ya kupata kiharusi (stroke). Wakati akitibiwa, madaktari waligundua kuwa alikuwa na shida kubwa ya kukojoa na walipomfanyia uchunguzi ndipo walipobaini kuwa ana jiwe hilo kubwa.

 

Daktari bingwa wa mfumo wa mkojo aliyeongoza upasuaji huo, Dkt. Pragaladhan Balakrishnan, ameeleza kuwa jiwe hilo lilichukua kati ya miaka 5 hadi 10 kukua na kufikia ukubwa huo ndani ya kibofu cha mgonjwa.

Rekodi ya awali ya jiwe kubwa zaidi la kibofu ilikuwa ya kilo 1.9 iliyowekwa nchini Brazil mwaka 2003.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet