pmbet

Maajabu, ndege mzee zaidi duniani ataga yai akiwa na miaka 74

Eric Buyanza

December 5, 2024
Share :

Ndege mzee zaidi duniani aliyepewa jina la Wisdom, ametaga yai akiwa na umri wa takriban miaka 74.

Wisdom alirekodiwa hivi karibuni na Shirika la Huduma ya Samaki na Wanyamapori la Marekani akitaga yai akiwa jirani na mwenzi wake mpya kando ya Bahari ya Pasifiki .

Inaelezwa na wanasayansi kuwa ndege wa aina hii kawaida huishi kwa miaka 12 mpaka 40, lakini Wisdom ni wa kipekee kwani alitambulishwa kwa jamii kwa mara ya kwanza mwaka 1956 alipokuwa na umri wa miaka mitano. 

Mtoto wake wa mwisho alitotolewa 2021 na mpaka amefikisha umri huu ameshakuwa na zaidi ya vifaranga 30.

Ukiachilia mbali mwenzi huyu mpya aliyenaye sasa, Wisdom ameshakuwa na wenzi wengine watatu katika maisha yake ambao inaaminika walikufa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet