Maalim Ayman wa Al-Shabab auawa
Eric Buyanza
December 23, 2023
Share :
Kiongozi wa wanamgambo wa Al-Shabaab, Maalim Ayman ameuawa na vikosi vya Somalia wakishirikiana na Marekani.
Waziri wa Habari wa Somalia, Daud Aweis amesema kiongozi huyo wa Al-Shabaab na kundi lake katika siku za karibuni walipanga kufanya mashambulizi nchini Somalia na Kenya.
“Imethibitishwa Maalim Ayman ameuawa katika operesheni ya pamoja ya Jeshi la Somalia kwa usaidizi wa vikosi vya Marekani tarehe 17 Disemba,” alisema Daud.
Ayman alikuwa kwenye orodha ya wanaotafutwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani huku zawadi ya Dola milioni 10 ikitolewa kwa taarifa zitakazopelekea kukamatwa kwake.