Maandamano dhidi ya Serikali ya Rais Ruto yashika kasi Kenya.
Joyce Shedrack
July 2, 2024
Share :
Baadhi ya wananchi Nchini Kenya wamejitokeza katika maeneo mbalimbali wakifanya maandamano yanayolenga kupinga Serikali ya Rais wa sasa wa Kenya William Ruto.
Maandamano hayo yameshika kasi siku ya leo katika miji mikubwa ya Nchi hiyo ikiwemo Jiji la Nairobi na Mombasa ikiwa ni siku chache tu tangu kuwepo kwa maandamo makubwa yaliyokuwa yanapinga Muswada mpya wa Fedha 2024.
Waliojitekeza wengi kwenye maandamano hayo ni kundi kubwa la vijana wenye umri mdogo maarufu kama Gen Z wanaosema bado hawajamalizana na Rais Ruto licha ya kuondosha muswada wa fedha waliokuwa wanaupinga kwenye maandamano ya wiki iliyopita.