MAANDAMANO KENYA: Barabara za kuingia Nairobi zafungwa
Eric Buyanza
July 7, 2025
Share :
Barabara zote za kuingia jijini Nairobi zimefungwa leo huku usalama ukimarishwa katika maeneo mbali mbali wakati ambapo maandamano yakitarajiwa kufanyika.
Vizuizi vimeonekana kwenye barabara kuu ambapo magari hayaruhusiwi kupita kuingia mjini na idadi kubwa ya polisi wameonekana katika maeneo mbali mbali ya jiji hilo.
Maeneo mengine yaliyowekwa vizuizi ni daraja la Kangemi, ambapo hata yale mabasi yaliyotoka safari kutoka nchi jirani hayaruhusiwi kupita, hivyo abiria wanalazimika kushuka na kutembea kwa miguu kuingia mjini au kutafuta mbinu nyingine za kufika makwao.
Vile vile, biashara nyingi zimefungwa katika barabara mbalimbali za mjini kama vile Moi Avenue.
BBC