pmbet

Maandamano yaibuka kwa mara nyingine Kenya.

Joyce Shedrack

July 13, 2024
Share :

Jeshi la polisi Nchini Kenya limelazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanyisha maelfu ya watu waliokuwa wamekusanyika mbele ya kituo cha polisi Kware Jijini Nairobi kufuatia kuokotwa kwa miili 9 ya watu karibu na kituo hicho cha polisi.

Wananchi hao waliojitekeza mbele ya kituo hicho walisikika wakiimba 'Ruto Must Go' wakionekana kuendelea kupinga Serikali ya Rais William Ruto licha ya mabadiliko makubwa aliyoyafanya ya kuvunja Baraza la Mawaziri.

Baadhi ya waandamanaji hao wameishutumu serikali kufuatia mauaji hayo huku wengi wakiwa na hofu juu ya baadhi ya watu ambao walipotea kwenye maandamo yaliyopita na mpaka sasa bado hawajapatikana.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet