Mabasi ya shule kuwa na walezi wawili, wakike na kiume
Eric Buyanza
May 24, 2024
Share :
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameelekeza mabasi yote ya shule yanayotumika kuwapeleka shuleni na kuwarudisha nyumbani wanafunzi lazima yawe na walezi wawili wa kike na wa kiume kila moja.
Mheshiwiwa Majaliwa ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Nancy Nyalusi, aliyehoji kama serikali haioni haja ya kutunga sheria ili kulinda usalama wa wanafunzi wanapokuwa kwenye magari.