Mabilionea wajenga makazi ya kifahari chini ya ardhi kukwepa vita
Eric Buyanza
August 27, 2025
Share :
Mabilionea ulimwenguni sasa wameanza mikakati ya ujenzi wa makazi ya kifahari ya 'chini ya ardhi' yaliyotengenezwa mahususi kabisa ili kuwalinda na hatari inayoweza kusababishwa na vita, athari za mabadiliko ya tabianchi au maafa makubwa yanayoweza kutokea.
Katika makazi haya ya kifahari ya chini ya ardhi mabilionea watapata huduma zote wanazozihitaji ikiwemo maji, umeme, hospitali, mahoteli nk.
Hivi majuzi, kampuni ya Kimarekani ya Safe ilitangaza mipango ya kujenga kitu walichokiita 'makao ya kimataifa' ambavyo ni vyumba vya chini ya ardhi zaidi ya 1,000 vitakavyokuwepo katika miji mbalimbali duniani.
Gharama za kutumia makazi haya itategemea ukubwa wa eneo utakalochagua.
Makazi ya mita za mraba 185, yatagharimu takriban dola milioni 2 (sawa na shilingi Bilioni 5 za kitanzania), lakini kwa makazi makubwa zaidi bei inaweza kufikia hadi dola milioni 20 (sawa na shilingi Bilioni 50 za kitanzania).