pmbet

Mabingwa wa safari Lager uso kwa uso na Yanga.

Joyce Shedrack

July 10, 2025
Share :

Kikosi cha Mbingwa wa Safari Lager Chenye wachezaji 22 watakaoiwakilisha Timu ya Mabingwa wa Safari Lager mwaka 2025  Wachezaji hao walichaguliwa kupitia mchakato wa kutafuta vipaji vya mpira wa miguu katika mikoa ya Mbeya, Arusha, Mwanza na Dar es Salaam.

Timu hiyo itakutana na Klabu ya Yanga (Yanga SC) katika fainali ya Kombe la Safari Lager siku ya Jumamosi, tarehe 26 Julai 2025, kwenye Uwanja wa KMC uliopo Mwenge.

 

Kombe la Safari Lager lilianzishwa mwaka Jana likiwa na lengo kuu la kuibua na kuinua vipaji vya soka vya vijana nje ya mfumo wa klabu za kitaalamu. Mashindano yalikuwa wazi kwa wachezaji wenye umri kati ya miaka 18 hadi 24 na yalifanyika kwa mfumo wa bonanza chini ya usimamizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

 

Safari Lager, wakishirikiana na makocha wabobezi pamoja na wawakilishi wa jamii kuwachambua wachezaji, hatimaye kupata timu inayojulikana kama Safari Champions iliyochaguliwa kwa kuzingatia uwezo wa kiufundi na ushiriki wa mashabiki kupitia tovuti maalum.

Khensani Mkhombo, Mkuu wa Masoko wa TBL, alisema kuwa mpango huu ulilenga kubadilisha mfumo wa kugundua vipaji vya soka nchini.

 

“Lengo letu katika Kombe la Safari Lager halikuwa tu kuandaa mashindano. Tulitaka kuunda tukio litakalobadili namna vipaji vya soka vinavyogunduliwa na kusherehekewa. Vijana hawa hawakusajiliwa — walionekana. Na makocha, mashabiki, na jamii zao. Hii ni timu iliyojengwa na watanzania”

 

Mechi ya mwisho ya Kombe la Safari Lager 2025 itafanyika kwenye Uwanja wa KMC, Dar es Salaam, siku ya Jumamosi tarehe 26 Julai ambapo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

 

Yanga SC, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na Safari Lager Cup, ambao pia wamenyakuwa Mataji mengine yote ya michuano ya ndani msimu huu, watakuwa timu pinzani katika mchezo huo. Klabu hiyo imeungana na Tanzania Breweries Limited katika kusaidia Kombe la Safari Lager mwaka huu kama sehemu ya juhudi za pamoja za kuendeleza soka la nyumbani.

 

Ali Kamwe, Meneja wa Mawasiliano na Habari wa Yanga SC, aliongeza:

“Huu si mchezo wa kawaida. Ni heshima, uwezo, na presha. Na tunaupokea kwa mikono miwili. Kama Yanga SC, tunaamini katika nguvu ya soka kuunganisha vizazi — na tunajivunia kuwa sehemu ya simulizi inayorudisha mpira kwa watu.”

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet