Mabinti wa vyuo wanauza mayai yao ya uzazi ili kujipatia pesa
Eric Buyanza
July 17, 2025
Share :
Daktari mmoja nchini Nigeria anayefahamika kwenye mtandao wa kijamii wa X kwa jina la Dr Penking ameelezea hofu yake juu ya kile alichokiita janga la 'Kimya Kimya', ambapo amedai kumekuwepo na ongezeko kubwa la idadi ya wanafunzi wa kike haswa wa vyuo vikuu kuuza mayai yao ya uzazi ili kujipatia fedha ya kujikimu.
Kwa mujibu wa Dakatari huyo, wanawake hawa wanakimbilia kwenye vituo vya uzazi na kuuza mayai yao kwa fedha ndogo jambo ambalo amesema linasababishwa na hali mbaya ya kiuchumi nchini humo.
"Wanawake wetu wadogo wanauza watoto wao wa baadaye kwa karanga kutokana na hali mbaya ya kiuchumi na kila mtu yuko kimya." aliandika kupitia mtandao wake wa X.
Maneno hayo yaliambatana na picha inayoonyesha mkono wenye glovu ukiwa umeshikilia kichupa kidogo chenye mirija kilichojazwa na kile kinachoonekana kuwa sampuli ya yai lililotolewa hivi karibuni.