Mabosi wa Unted wampata mrithi wa Ten Hag
Sisti Herman
May 24, 2024
Share :
Mabosi wa klabu ya Manchester United inaangalia uwezekano wa kumpata kocha mkuu wa klabu ya Ipswich Kieran Mckenna kwaajili ya kurithi mikoba ya Erik Ten Hag ambaye mpaka sasa mguu moja upo ndani mwingine ukiwa nje kuendelea kuwa kocha wa United.
McKenna aliwahi kuwa kocha msaidizi wa United kipindi cha Ole Gunnar Solskjærl lakini pia kocha wa timu za vijana hivyo kama atarejea Old Trafford hatakuwa mgeni.
Mabosi wa United chini ya tajiri Sir Jim Ractliffe wapo kwenye msako mkali kutafuta kocha atakayewapeleka nchi ya ahadi ambapo awali tetesi zilianza kwa Thomas Tuchel pia.