Mabosi wapya Man Utd wamkaushia kocha wa Ronaldo
Sisti Herman
April 16, 2024
Share :
Kocha wa washambuliaji wa klabu ya Manchester United Benni McCarthy raia wa Afrika Kusini mkataba wake kuitumikia klabu hiyo unaelekea ukingoni na hadi sasa hajaongezewa mkataba mpya ikiwa ni tafsiri ya kutokuendelea na mradi mpya chini ya tajiri mpya wa klabu hiyo ambaye Sir Jim Ractliffe ambaye anadaiwa kupitisha 'fagio' mwishoni mwa msimu.
Benni ambaye pia ndiye mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya Afrika kusini akiwa na mabao 31 alijiunga na United kama mmoja wa wasaidizi wa Erik Ten Hag Julai 2022 akiwa na jukumu la kuwanoa washambualiaji kama Cristiano Ronaldo na Marcus Rashford.
Benni alianzia ukocha nchini Afrika kusini kunako klabu ya Amazulu.