Mabosi Yanga waweka mzigo mezani, Belouizdad lazima wapasuke!
Eric Buyanza
February 24, 2024
Share :
Yanga leo inakutana na CR Belouizdad katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, mchezo ambao Yanga wameupa jina la ‘Pacome Day’.
Taarifa iliyotifikia mezani ni kwamba, mabosi wa klabu hiyo kongwe nchini wameweka mezani kitita kisichopungua milioni 500 kama hamasa kwa wachezaji wa timu hiyo walioahidi kupambana kwa jasho na damu ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi pale Uwanja wa Benjamin Mkapa usiku wa leo.
Kwa hali inavyoonekana, Yanga na uongozi mzima wa klabu hiyo wamepania mno kuhakikisha klabu hiyo safari hii wanacheza robo fainali ya michuano hiyo mikubwa kwenye ngazi ya klabu hapa Afrika.
Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amesema wanakwenda kucheza mechi ambayo lazima washinde na hakuna tafsiri nyingine.