Machi 21 tutamjua mbabe wa Taifa kati ya Vunjabei na Sarah Alex
Sisti Herman
March 18, 2026
Share :

Baada ya kuumaliza mwaka 2025 kwa kuwachapa mabondia wakali kama Stumai Muki na Zulfa Iddy kwenye mapambano yake yaliyopita, Bondia namba 1 kwasasa kuliko wote Tanzania Sarah Alex atapanda ulingoni na Bondia namba 2 kwasasa Halima Vunjabei usiku wa machi 21, 2026.
Sarah Alex aliingia rasmi kwenye orodha ya mabondia 10 bora barani Afrika kwa uzito wa Super Bantam baada ya kumchapa Stumai Muki na kushinda kwa uamuzi wa majaji watatu kati ya wanne.
Kwa mujibu wa orodha rasmi ya mtandao wa kukusanya, kutunza na kuhifadhi takwimu za mapambano ya Mabondia, Boxrec, kwa uzito wa Super Bantam, kuanzia kilo 54.4 hadi 55.3, Sarah Alex anashika nafasi ya 7 barani Afrika, na nafasi ya kwa kwanza kwa Mabondia wa kike Tanzania, akifuatiwa na bondia Halima Vunjabei.





