pmbet

Machinga sasa kupewa mikopo bila dhamana

Eric Buyanza

April 12, 2024
Share :

Wafanyabiashara wadogo, maarufu kama Machinga, ambao wamekuwa wakifanya shughuli zao kwenye maeneo yasiyo rasmi yakiwamo hifadhi za barabara, wameshauriwa kuhamia kwenye masoko rasmi ili wanufaike na fursa mbalimbali ambazo zinatolewa na serikali.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa, alitoa ushauri huo juzi kwenye uzinduzi wa mpango maalumu wa mikopo bila dhamana kwa wafanyabiashara walioko katika maeneo rasmi, wakiwamo walioko kwenye masoko jijini Mbeya. Mpango huo umeanzishwa na benki ya CRDB.

Alisema ili kuwaepusha wafanyabiashara hao na adha mbalimbali, serikali imewapangia maeneo ambayo yameandaliwa yakiwamo masoko lakini bado wanaonekana wakirandaranda kwenye maeneo ya barabarani.

Eneo la uwanja wa zamani wa ndege wa Mbeya, alisema limetengwa eneo maalumu kwa ajili ya machinga na baadhi yao wamejenga vyumba vya biashara na wanaendelea na shughuli zao bila bughudha.

“Hii ni fursa muhimu kwenu wajasiriamali wetu. Ingieni kwenye masoko hayo mfanye kazi zenu na mpate pia fursa ya mikopo yenye masharti nafuu katika orodha ya masoko hayo hata soko hili la uwanja wa ndege limo,” alisema.

Meneja Masoko wa CRDB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Japhar Hasanali, alisema lengo la kuanzisha mpango huo ni kuwaepusha wafanyabiashara hao na mikopo inayotolewa na taasisi zisizo rasmi ambayo ina riba kubwa maarufu kwa jina la ‘kausha damu’.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet