pmbet

Macron: Trump ametoa kauli ya kipumbavu kuhusu waislam

Sisti Herman

October 23, 2026
Share :

 

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amekosoa matamshi ya Rais wa Marekani, Donald Trump, na viongozi wengine wa kigeni wanaowalaumu wahamiaji Waislamu kwa machafuko nchini Ufaransa, akiyataja kuwa ya kipumbavu.

Macron amesema hakukuwa na dalili za wazi za uingiliaji wa moja kwa moja wa kigeni katika matukio hayo, lakini amedai kuwa taarifa za kupotosha, zikiwemo picha zilizotengenezwa kwa akili bandia (AI), zilitumika kuonyesha matukio ambayo hayakutokea nchini humo.

Aidha, amekanusha madai kwamba Ufaransa imefurika makundi ya wahamiaji na wenye misimamo mikali ya Kiislamu, akiwakosoa viongozi wanaoizungumzia nchi hiyo vibaya. “Watu hao wananikera. Mimi ninaipenda nchi yangu,” amesema Macron.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet