pmbet

Madaktari walimwambia ulikuwa muujiza kwake kuishi tena jana ameibeba Mexico.

Joyce Shedrack

June 12, 2026
Share :

Mshambuliaji wa Mexico, Raúl Jiménez ameandika moja ya simulizi za kuvutia zaidi katika soka la kisasa baada ya kupitia nyakati ngumu na kufanikiwa kuzishinda zisizuie ndoto zake.

First, Raul Jimenez survived. Then he thrived. And now he has done it at a  World Cup - The Athletic

Novemba mwaka 2020 akiwa mchezaji wa Wolverhampton Wanderers katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Arsenal Jiménez alipata jeraha baya la kichwa baada ya kugongana kwa nguvu na beki David Luiz. 

 

Ajali hiyo ilisababisha kupasuka kwa fuvu la kichwa (skull fracture), hali iliyohitaji upasuaji wa haraka na matibabu maalumu. Madaktari walieleza kuwa jeraha hilo lilikuwa kubwa kiasi kwamba maisha yake yalikuwa hatarini huku wakiweka wazi kuwa ilikuwa muujiza kwa nyota huyo kuendelea kuwa hai.

 

Baada ya miezi mingi ya matibabu na mazoezi ya kurejea uwanjani, Jiménez alifanikiwa kupona na kuendelea na maisha yake ya soka akiitumikia klabu ya Fulham ambako aliendelea kuonyesha kiwango kizuri na kuthibitisha kuwa bado ni mmoja wa washambuliaji muhimu wa Mexico.

 

Mwaka 2026 ulimletea changamoto nyingine nje ya uwanja baada ya kumpoteza baba yake mpendwa, jambo lililomuumiza sana kihisia. 

 

Katika mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Dunia 2026 uliochezwa kwenye Estadio Azteca, Jiménez aliiongoza Mexico kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Afrika Kusini akiandika historia kwa kufunga bao lake la kwanza kabisa katika Kombe la Dunia.

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet