pmbet

Madaktari waonya 'Shisha' kuleta majanga baada ya miaka michache

Eric Buyanza

June 6, 2024
Share :

Madaktari bingwa wameonya kwamba miaka michache ijayo, Tanzania itakuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wa moyo na saratani kwa watu wenye umri mdogo, kama matumizi ya shisha yataendelea kwa kasi iliyopo. 

Wakizungumza kwenye kipindi cha Malumbano ya Hoja kinachorushwa na kituo cha ITV, wamesema takwimu za kimataifa zinaonyesha zaidi ya nusu ya watumiaji wa tumbaku hufariki kabla ya wakati.

Bingwa wa magonjwa ya mfumo wa upumuaji kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Mwanaada Kilima, amesema asilimia 90 ya saratani ya mapafu na koo inatokana na matumizi ya tumbaku wakati bidhaa hizo zikichangia asilimia 40 ya aina nyingine ya saratani.

“Nimeona madhara mengi na makubwa sana…matumizi ya tumbaku ya aina yoyote ile iwe ya kusokota, kumung’unya, sigara au za kielektroniki ni majanga. Ukichukua takwimu za Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), utaona namna tumbaku inavyochochea saratani,” amesema.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet