Madeni yaiponza Fountain Gate Fc yafungiwa usajili.
Joyce Shedrack
July 26, 2024
Share :
Klabu ya Fountain Gate zamani Singida Fountain Gate FC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara imefungiwa kufanya usajili mpaka itakapomlipa aliyekuwa kocha wake Thabo Senong.
Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ limetoa taarifa inayoeleza uamuzi huo uliofanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) baada ya kocha huyo raia wa Afrika Kusini kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo.
Senong alifungua kesi FIFA akidai malipo ya malimbikizo ya mishahara na fidia ya kuvunjiwa mkataba kinyume na taratibu.
Klabu ya Fountain Gate (Singida Fountain Gate FC) ilitakiwa iwe imemlipa kocha huyo ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa lakini haikutekeleza hukumu hiyo hivyo imefungiwa kufanya usajili mpaka pale itakapokamilisha malipo ya kocha huyo.