pmbet

Madereva bodaboda shirikini kutoa taarifa za uhalifu

Eric Buyanza

April 16, 2026
Share :

Madereva wa pikipiki, maarufu bodaboda, wa Mtaa wa Ziwani, Kata ya Pasiansi mkoani Mwanza, wametakiwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu ili kuimarisha ulinzi na usalama.

 

Wito huo umetolewa Aprili 14, 2026 na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Ilemela, Mkaguzi wa Polisi Stephano Mcha, alipokuwa akizungumza na madereva hao katika mtaa huo kwa lengo la kutoa elimu ya usalama.

 

Alisema ajali nyingi husababishwa na uzembe, ikiwemo kutofanya ukaguzi wa mara kwa mara wa pikipiki, na kusisitiza umuhimu wa kufuata sheria za barabarani.

Aidha, aliwahimiza bodaboda hao kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za vitendo vya uhalifu ili kusaidia kupunguza matukio hayo na kuimarisha usalama katika jamii.

 

@polisi.tanzania

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet