pmbet

Madiwani Iringa waomba kondomu kwa wingi

Eric Buyanza

February 28, 2024
Share :

Ongezeko la uzalishaji wa pombe ya kienyeji aina ya ulanzi umehusishwa kwa kiwango kikubwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) nkoani Iringa.
 

Hali hiyo imewaibua baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wakitaka usambazaji wa kondomu katika vilabu vinavyouza pombe hiyo kuongezwa.
 

Madiwani hao wameiomba kamati ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Ukimwi kuhakisha mipira hiyo ya kiume haikosekani katika maeneo hayo ya vilabu vya pombe na maeneo mengine hatarishi.
 

“Ulanzi ni moja ya kilevi ambacho tafiti mbalimbali zinaonesha kimekuwa kichocheo cha ngono zisizo salama na matokeo yake ni ongezeko la maambukizi ya VVU na magonjwa mengine ya ngono. ” alisema mmoja wa madiwani hao, Vumilia Mwenda.
 

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo, Ihemi, Mwenda alisema kuna ongezeko kubwa la uzalishaji wa pombe hiyo katika kipindi hiki cha mvua za masika.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet