Madrid ilipocheza dhidi ya Madrid fainali ya Copa Del Rey 1980
Sisti Herman
November 15, 2026
Share :

Mnamo mwaka wa 1980, Real Madrid ilifika fainali ya Copa del Rey na mpinzani wake alikuwa Real Madrid.
Castilla, timu ya akiba ya klabu hiyo inayocheza ligi daraja la pili, iliwaondoa Athletic Bilbao, Real Sociedad na Sporting Gijón kwenye hatua za awali za mtoano kabla ya kufika fainali.
Kisha wakajitokeza uwanjani Bernabéu kukabiliana na Real Madrid yenye wale wachezaji ambao waliota ndoto ya kucheza nao pamoja.
Timu ya kwanza ilishinda kwa mabao 6-1. Lakini hadithi haikuishia hapo: Castilla ilikwenda barani Ulaya na kuifunga West Ham mabao 3-1.





