Madrid kumfanya Mbappe mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi
Eric Buyanza
May 11, 2024
Share :
Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe mwenye umri wa miaka 25, atakuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi Real Madrid ikiwa atasaini na klabu hiyo baada ya kuondoka Paris Saint-Germain.
Kulingana taarifa Mbappé anaenda kuwazidi mshahara Vinicius Junior pamoja na Jude Bellingham.
Kwasasa wawakilishi wa Mbappe wanashinikiza kupata sehemu kubwa zaidi ya (haki za picha).