Madrid waiambia Liverpool, "tunamtaka Alexander-Arnold"
Eric Buyanza
November 30, 2024
Share :
Miamba ya Hispania, Real Madrid wameifahamisha klabu ya Liverpool ya Uingereza kuhusu nia yao ya kutaka kumsajili beki wa kulia Trent Alexander-Arnold.
Hata hivyo, duru za karibu na mabingwa hao wa Ulaya zinasema wanataka kulifanya jambo hilo kwa utaratibu mzuri na heshima kubwa bila kuwakwaza Liverpool.
Kwa upande wa Liverpool bado wana matumaini makubwa ya kuweza kumshawishi beki huyo aweze kusaini mkataba mpya Anfield.
Alexander-Arnold amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu kwenda Real Madrid.