Madrid watwaa Ubingwa Hispania
Sisti Herman
May 5, 2024
Share :
Baada ya klabu ya Barcelona kufungwa 4-2 na Girona jana usiku kwenye mchezo wa ligi kuu nchini Hispania, klabu ya Real Madrid imetawazwa kuwa mabingwa wa ligi hiyo kwa mara ya 36.
Kabla ya mechi ya Girona na Barca, Madrid walikuwa na mechi dhidi ya Cadiz na kushinda 3-0.
Madrid wametwaa ubingwa huo baada ya kufikisha alama 87 baada ya michezo 34 wakiwazidi Girona na Barcelona ambao wana alama 74 na 73 kiasi ambacho kwa idadi ya mechi zilizobakia haziwezi kuzifikia alama za Mabingwa hao wa Ulaya na Hispania.