Madrid yaikomalia Bayern kwao
Sisti Herman
May 1, 2024
Share :
Klabu ya Real Madrid jana imefanikiwa kulazimisha sare ya 2-2 ugenini kwa Bayern Munich kwenye mchezo wa nusu fainali ya ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kwenye mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la Allianz Arena mabao ya Madrid yalifungwa na winga hatari raia wa Brazil Vinicius Jr huku yale ya Bayern yakifungwa na mshambuliaji mwingereza Harry Kane na winga Leroy Sane.
Baada ya sare hiyo Madrid imerahisisha kazi ya ugenini na sasa inasubiri kumaliza kwenye mchezo wa nyumbani.