Madrid yapunguza mshahara wa Mbappe
Sisti Herman
February 16, 2024
Share :
Baada ya jaribio la kuhitaji kumsajii mshambuliaji wa PSG na timu ya Taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe mwaka 2022 kukwama baada ya mshambuliaji huyo hatari kusaini dili na PSG wakati huo, Real Madrid tayari wametuma pendekezo la mkataba mwingine kwenye kambi ya Kylian Mbappé baada ya mshambuliaji huyo juzi kuujulisha uongozi wa PSG kuwa huu utakuwa msimu wa mwisho na mabingwa hao mara 6 mfululizo wa ligi kuu Ufaransa.
Madrid imewasilisha pendekezo hilo ikiwa na imepunguza mshahara kwa asilimia nyingi kulinganisha na kiasi walichowasilisha kwa Mbappe majira ya joto ya mwaka 2022.