pmbet

Maelfu waingia barabarani nchini Venezuela kupinga matokeo ya uchaguzi

Eric Buyanza

July 30, 2024
Share :

Vikosi vya usalama nchini Venezuela vimerusha mabomu ya machozi na risasi za mpira dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakipinga matokeo ya uchaguzi nchini humo. 

Maelfu ya watu walikusanyika katikati ya mji wa Caracas Jumatatu jioni, wengine wakitembea umbali mrefu kutoka vijijini kwenye milima inayozunguka jiji hilo, kuelekea ikulu ya rais. 

Maandamano hayo yalizuka siku moja baada ya Rais Nicolas Maduro kudai kuwa ameshinda. Upinzani umepinga ushindi wa Bwana Maduro na kuuchukulia kama ulaghai, ukisema mgombea wake Edmundo González alishinda kwa kishindo kwa kupata asilimia 73.2 ya kura. 

Kundi kubwa la wanajeshi na polisi, ikiwemo mabomu ya kutoa machozi, walionekana kwenye mitaa ya Caracas kwa lengo la kujaribu kuwatawanya waandamanaji na kuwazuia kukaribia ikulu ya rais. Umati wa watu uliimba “Uhuru, uhuru!” na kuitaka serikali kuang’atuka madarakani.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet