Maestro amvulia kofia Mzize
Sisti Herman
April 11, 2024
Share :
Mara baada ya kutupia bao kali nyavuni kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Dodoma jiji ugenini, mshambuliaji kinda wa klabu ya Yanga Clement amepongezwa na aliyekuwa mchezaji wa zamani ambaye kwasasa ni mchambuzi na mtangazaji wa vipindi vya michezo kupitia EFM na TVE Ibrahim Masoud "Maestro" amempongeza na kumtia moyo huku akiwa na matumaini makubwa na yeye siku za usoni.
"Mimi ni shabiki yako mwana, ipo siku utaimbwa, Keep it up (endelea kukaza)" aliandika Maestro kupitia mtandao wake wa Instagram.
Maestro aliyasema hayo akiambatanisha na video ya goli la Mzize alilofunga dhidi ya Dodoma jiji Yanga wakishinda 2-0 huku goli lingine wakijifunga Dodoma baada ya krosi chonganishi ya Augustine Okrah.