pmbet

Mafia wa Simba aliyetangulia amaliza mambo!

Eric Buyanza

December 5, 2023
Share :

Klabu ya Simba leo saa 9 alasiri imeanza safari kuelekea nchini Morocco katika jiji la Marakech kwaajili ya mchezo wa raundi ya pili ya ligi ya mabingwa Afrika barani Ulaya dhidi ya Wydad Athletic Club.
 

Meneja habari na mawasiliano wa klabu hiyo Ahmed Ally asubuhi ya leo kwenye mazoezi ya mwisho ya timu hiyo amethibitisha kuwa mratibu wa timu hiyo Abas Ally na baadhi ya viongozi wengine walishatangulia Morocco kuwekaa mazingira sawa

"Abbas alishatangulia kuweka mambo sawa kuhakikisha masuala ya usafiri, malazi na miundombinu ya mazoezi iko sawa, hadi sasa tupo salama" alisema Ahmed.
 

Simba wapo nafasi ya tatu kundi B ikiwa na alama 2 baada ya sare mbili mfululizo kwenye micezo miwili ya mwanzo ya kundi hilo dhidi ya Asec Mimosas na Jwaneng' Galaxy na wanaenda kukutana Wydad inayoburuza mkia wa kundi baada ya kupoteza michezo yote ya mwanzo.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet