Magereza yafungwa Uholanzi, kutokana na uhaba wa wafungwa!
Eric Buyanza
February 21, 2024
Share :
Kutokana na kupungua kwa viwango vya uhalifu, Uholanzi inapanga kufunga magereza kadhaa katika miaka ijayo.
Inaelezwa kuwa program zinazotolewa magerezani na sehemu mbalimbali kwa ajili ya kurekebisha tabia kwa wahalifu imekuwa chachu kubwa ya kupunguza uhalifu nchini humo.
Uholanzi imeshuhudia kupungua kwa viwango vya uhalifu kwa mwaka hadi kufikia asilimia 0.9%
Mwenendo huu mzuri uliwezesha kufungwa magereza 8 mwaka 2009 na mengine 19 yalifungwa mwaka 2014 na bado zoezi hilo la kuendelea kuyafunga linaendelea.