pmbet

Magereza yageuzwa hoteli uholanzi baada ya kukosa wafungwa

Eric Buyanza

May 4, 2026
Share :

Magereza nchini Uholanzi yanageuzwa kuwa mahoteli, ofisi, na vituo vya kitamaduni kutokana na upungufu mkubwa wa wafungwa. Tangu mwaka 2014, nchi hiyo imefunga zaidi ya magereza 23 kwa sababu jela nyingi nyingi zimebaki tupu.
 

Mbali na hoteli, magereza mengine yametumika kama makazi ya muda ya wakimbizi na vituo vya biashara ili kuhakikisha majengo hayo yanabaki na matumizi yenye tija kwa jamii.
 

Viwango vya uhalifu nchini humo vimeshuka kwa kiasi kikubwa, hasa makosa ya wizi na vurugu.

 

Mahakama za Uholanzi sasa zinapendelea kutoa adhabu mbadala kama faini, huduma za jamii, na ufuatiliaji wa kielektroniki badala ya vifungo vya gerezani.

 

Serikali imeweka mkazo zaidi katika kuwarekebisha wahalifu na kuwarudisha kwenye jamii (rehabilitation) badala ya kuwaadhibu kwa kuwafunga.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet