pmbet

"Magufuli alijua hatapona, akasema arudishwe akafie nyumbani" - Jen. Mabeyo

Sisti Herman

March 17, 2024
Share :

Leo imetimia miaka mitatu tangu kufariki kwa aliyekuwa Rais wa awamu ya 5 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli aliyefariki machi 17 mwaka 2021.

 

Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Venance Mabeyo kwenye mahojiano maalum Waandishi wa Habari kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) ikiwa sehemu ya kumbukumbu ya siku hii, amesema siku moja kabla ya kifo cha Hayati John J. Magufuli, alimwita na kumwambia anajua hawezi kupona na hivyo awaagize madaktari wamrudishe nyumbani kwake.

Mabeyo amesema “aliniita CDF njoo, siwezi kupona, waamuru hawa Madaktari wanirudishe nyumbani. Nikamjibu Mheshimiwa sina Mamlaka hayo, suala la Afya sio la CDF, naomba ubaki madaktari watatuambia”

Katika Makala CDF ameongeza kuwa Machi 17, 2021 saa 8 mchana, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama waliambiwa hali ya Rais Magufuli imebadilika na ilipofika saa 12:30 Jioni alifariki.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet