pmbet

Mahakama: Donnarumma na mkewe walivamiwa

Sisti Herman

September 11, 2026
Share :

 

Mahakama ya jinai nchini Ufaransa imewakuta na hatia majambazi waliovamia nyumbani wa Kipa Gianluigi Donnarumma na mke wake, Alessia Elefante, waliokuwa wahanga wa uvamizi wa kutisha nyumbani kwao jijini Paris mnamo Julai 2023, ambapo walifungwa kamba na kutishiwa kwa kisu wakati mwanamke huyo akiwa mjamzito.

Maelezo hayo ya kushtusha yalifunuliwa hivi karibuni mbele ya mahakama ya jinai nchini Ufaransa wakati wa kesi ya watuhumiwa wa tukio hilo.Wizi huo ulitokea usiku wa manane wakati wanandoa hao wakiwa wamelala kwenye ghorofa yao iliyopo mtaa wa kifahari wa Avenue Montaigne.

Majambazi walivunja dirisha na kuingia ndani, ambapo walimfunga Donnarumma na kumpiga usoni kwa ngumi ya chuma, huku Elefante akishuhudia kuwa walimvuta nywele na kumpiga mapajani licha ya kuwaambia alikuwa mjamzito.

Washambuliaji hao walitoroka na vitu vya thamani vya karibu Euro 500,000 (zaidi ya shilingi bilioni 1.5 za Kitanzania), vikiwemo saa za kifahari, mikoba ya wabunifu, na pesa taslimu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet