pmbet

Mahakama Kenya yaidhinisha kutumika kwa Jeshi kutuliza ghasia

Eric Buyanza

June 28, 2024
Share :

Mahakama nchini Kenya jana jioni iliidhinisha uamuzi wa kulipeleka jeshi mitaani kuwasaidia polisi, wakati maandamano yakiendelea dhidi ya mswada tata wa kodi ambao serikali imeahidi kuuondoa.

Mahakama ilitoa uamuzi huo na kusema hatua ya kutumiwa jeshi iliyoidhinishwa na bunge, ni ya halali kutokana na kuzuka kwa machafuko wakati wa maandamano, ambayo polisi wameshindwa kuyadhibiti. 

Mahakama hiyo pia ilipinga rufaa iliyowasilishwa na chama cha wanasheria.

Hata hivyo Jaji Lawrence Mugambi alionya kuhusu kile alichosema mwenendo hatari ambao huenda ukasababisha nchi kuwa chini ya udhibiti wa jeshi. 

Kwa hiyo ametaka taarifa sahihi kutoka kwa serikali kuhusu ni namna gani jeshi litatumika na kwa muda gani.

Alhamisi kulishuhudiwa maandamano katika maeneo tofauti ya nchi ukiwemo mji mkuu Nairobi. 

Kulikuwa na ulinzi mkali hasa katika eneo la Ikulu baada ya waandamanaji kusema walipanga kuandamana hadi Ikulu ya Rais. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet