Mahakama yapiga marufuku kurusha 'LIVE' kesi ya Tundu Lissu.
Joyce Shedrack
August 18, 2025
Share :
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepiga marufuku kurushwa kwa matangazo ya moja kwa moja (live) ya kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu ili kulinda taarifa za mashahidi.
Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Franco Kiswaga ameeleza hayo mahakamani hapo siku ya leo akiweka wazi kuwa urushaji wa matangazo ya moja kwa moja wa kesi ya Lissu umezuiwa hadi pale amri nyingine itakapotolewa na Mahakama hiyo au Mahakama Kuu.
"Uchezaji wa moja kwa moja au live streaming, utangazaji, usambazaji wa moja kwa moja mtandaoni au aina nyingine ya uenezaji wa moja kwa moja kwa umma yaani ukijumuisha mitandao ya kijamii au matangazo ya video wakati wa mchakato mzima wa usomaji wa maelezo ya awali ya kesi (commital proceeding) hii, Mahakama inavizuia hadi pale itakapotolewa amri nyingineyo na Mahakama hii au Mahakama Kuu." amesema Kiswaga.