pmbet

Mahakama yasema Trump ana kinga, hatashitakiwa

Eric Buyanza

July 2, 2024
Share :

Mahakama Kuu nchini Marekani imetoa uamuzi kwamba Rais wa zamani wa nchi hiyo Donald Trump hawezi kufunguliwa mashtaka kwa vitendo ambavyo vilikuwa ndani ya mamlaka yake ya kikatiba wakati akiwa rais.

Uamuzi huo huenda ukachelewesha kesi yake ya kula njama ya kutaka kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020. 

Uamuzi huo wa majaji wa mahakama ya juu umetolewa miezi minne kabla ya uchaguzi wa rais ambapo Trump atakabiliana na Joe Biden.

Jaji Mkuu Mhafidhina John Roberts, alisema kuwa rais "hayuko juu ya sheria" lakini ana "kinga kamili" dhidi ya kufunguliwa mashitaka ya jinai kwa matendo yanayofanyika pindi akiwa madarakani.

Majaji ambao hawakukubaliana na uamuzi huo, wamekosoa vikali na kuibua wasiwasi juu ya mustakabali wa kidemokrasia wa nchi hiyo. 

Trump ameutaja uamuzi huo kuwa ni "Ushindi mkubwa."

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet