Mahakama yatengua uamuzi wa Baraza Kuu la CHADEMA
Eric Buyanza
December 14, 2023
Share :
Mahakama Kuu imetengua uamuzi wa Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lililoidhinisha uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho uliowavua uanachama Halima Mdee na wenzake 18
Akisoma hukumu hiyo Jaji Cyprian Mkeha amesema kitendo cha wajumbe wa kamati kuu iliyowafukuza kuwa tena wajumbe wa Baraza Kuu ambalo lilisikiliza rufaa yao kinaondoa uhalali wa maamuzi ya Baraza Kuu. Baraza Kuu lilikwenda kinyume na kanuni ya kawaida ya kutokupendelea (The Law of Impartiality).