pmbet

Mahakama yatupilia mbali kesi ya Jay Z.

Joyce Shedrack

July 2, 2025
Share :

Taarifa zinasema kuwa Jaji wa California ‘Mark Epstein’ ameitupilia mbali kesi ambayo Jay-Z alimfungulia wakili wa Texas ‘Tony Buzbee’, wakili ambaye alimshtaki Jayz kwa kumnyanyasa kingono mtoto wa miaka 13 katika tukio la Mwaka 2000 pamoja na Sean “Diddy” Combs.

Rapa huyo alituhumiwa kubaka binti wa miaka 13 mwaka 2000, na kisha baadae kukanusha madai hayo akidai kusikitishwa na mwanasheria ambaye amefungua shtaka hilo huku bila kupepesa macho akiliita shtaka hilo kuwa ni upuuzi na lilikuwa na lengo la kumkamua pesa na kumdhalilisha tu. hata hivyo Jay z alishinda kesi hiyo aliyodai kuwa imejaa uzushi na hadithi za kutunga na baadae kumgeuzia kesi Buzbee kwa kumchafua.

Nhạc Cụ Tất Thắng
Jay-Z katika Shtaka lake alidai tuhuma hizo zimechafua taswira yake kwani Buzbee na wakili mwenzake David Fortney walifungua kesi hiyo wakijificha nyuma ya mgongo wa binti kwaajili ya faida zao binafsi.

Hivyo Jaji Mark Epstein hajaridhishwa na madai hayo ya Jay-Z kuchafuliwa na Buzbee na hivyo kuifuta kesi hiyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet