Mahakama yawahukumu kunyongwa Masheikh 6 Arusha
Eric Buyanza
December 13, 2023
Share :
Mahakama kuu Kanda ya Arusha imewasomea mashtaka masheikh 9 miongoni mwa wanaoshikiliwa kwa zaidi ya Miaka 10 katika Gereza kuu la Kisongo.
Masheikh 6 kati yao wamekutwa na hatia ya kulipua Kanisa Katoliki la Parokia ya Mtakatifu Joseph Olasiti Mwaka 2013 na kusababisha madhara makubwa hivyo kuhukumiwa kunyongwa.
Waliohukumiwa ni Imam Jaafar Hashima Lema, Yusuf Ali Huta, Ramadhani Hamadi Waziri, Abdul Hassa Masta, Kassim Idrisa na Abashari Hassan Omari na waliochiwa huru ni Abduli Humud Wagoba, Abdurahmani na Amani Mussa Pakasi (ambaye amerejeshwa gerezani kwa kosa lingine).