pmbet

Mahakama yazuia kiongozi wa upinzani kugombea Urais Rwanda

Eric Buyanza

March 23, 2024
Share :

Mahakama ya juu nchini Rwanda, imemzuia Kiongozi wa upinzani nchini humo, Victoire Ingabire, kuwania kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika baadaye Julai 15 mwaka huu.

Majaji wa mahakama hiyo mjini Kigali wametupilia mbali ombi la Ingabire akitaka kurejeshewa haki yake ya kiraia na hivyo kumzuia kugombea katika uchaguzi wa urais baadae mwaka huu.

Inaelezwa kuwa kiongozi huyo ameiambia DW kwamba hata hivyo aliheshimu masharti yote yaliyowekwa baada yeye kuachiliwa huru kwa msamaha wa rais mwaka 2018.

Victoire Ingabire amesema uamuzi huu wa mahakama si jambo la kushangaza kwa sababu serikali ya Kigali haitaki upinzani unaoaminika.

''Chama tawala, RPF, hakiko tayari kuwapa nafasi wapinzani, hakiko tayari kushindana na wengine ambao wana sera ambayo Wanyarwanda wanaweza kupata fursa ya kuchagua,” amesema Ingabire na kuongeza;

“Kwa hivyo chama cha RPF hakiko tayari kukubali ushindani. Lakini wakati huo huo, Wanyarwanda wana kiu ya demokrasia, wana kiu ya kuwa na nchi ambayo inaweza kujieleza kwa uhuru.''

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet