Mahakamani kwa kuua mtu na kula viungo vyake
Eric Buyanza
May 2, 2024
Share :
Jamaa mmoja aliyetambulika kwa jina la Colin Czech ameburuzwa Mahakamani huko Las Vegas nchini Marekani baada ya kudaiwa kumpiga na kumuua mtu aliyefahamika kwa jina Kenneth Brown na kisha kula viungo vyake (sikio na jicho).
Tukio hilo linadaiwa kutokea Jumapili ya Aprili 28 kwenye kituo cha basi na polisi walipofika eneo hilo walimkuta Kenneth akiwa anavuja damu nyingi na baada ya muda alifariki.
Colin amefikishwa mahakamani leo May 2.