Maharamia wa kisomali wateka meli ya mizigo
Eric Buyanza
August 18, 2026
Share :

Maharamia wameiteka meli ya mizigo karibu na pwani ya Somalia, katika tukio la hivi karibuni kufuatia kuongezeka kwa mashambulizi ya baharini katika eneo la Pembe ya Afrika.
Mashirika yanayofuatilia usalama wa baharini yamesema watu wanane waliingia ndani ya meli hiyo karibu na Marraye na kutwaa udhibiti wake. Jina la meli halijatajwa, lakini wafanyakazi wake wameripotiwa kuwa salama.
Uharamia katika pwani ya Somalia ulifikia kilele mwaka 2011 kabla ya kupungua kutokana na operesheni za kimataifa.
Hata hivyo, mashambulizi yameongezeka tena mwaka huu. Tangu Aprili, meli kadhaa zilizobeba mafuta, mbolea na kemikali zimetekwa. Matukio hayo yanaongeza hatari kwa usafirishaji katika Bahari ya Shamu.
DW





