MAhmed Arajiga ateuliwa kuchezesha mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika.
Joyce Shedrack
October 6, 2026
Share :
Mwamuzi wa kimataifa wa Tanzania, Ahmed Arajiga, ameteuliwa na CAF kuwa mwamuzi wa mchezo wa mkondo wa kwanza wa raundi ya pili ya mchujo wa CAF Champions League kati ya Star Sport Academy ya Sierra Leone na RS Berkane ya Morocco.

📅 Tarehe: 17 Oktoba 2026
📍 Uwanja: Samuel Kanyon Doe Sports Complex, Paynesville, Liberia
⏰ Muda: Saa 4:00 usiku kwa saa za Tanzania (16:00 GMT)
Mchezo huo umehamishiwa Liberia kutokana na kutokuwepo kwa uwanja uliothibitishwa na CAF nchini Sierra Leone kwa ajili ya kuandaa mchezo huo.
Arajiga, ambaye amekuwa mwamuzi wa kimataifa wa FIFA tangu 2022, anaendelea kupewa majukumu katika mashindano ya kimataifa chini ya CAF na FIFA.





