pmbet

Mahujaji 14 wafariki kutokana na joto kali Saudi Arabia

Eric Buyanza

June 17, 2024
Share :

Takriban mahujaji 14 kutoka Jordan wamefariki dunia kutokana na joto kali wakati wa ibada ya Hijja nchini Saudi Arabia. 

Wizara ya mambo ya nje ya Jordan imesema jana kuwa mahujaji wengine 17 hawajulikani waliko. Awali, wizara hiyo ilithibitisha vifo vya mahujaji sita raia wa Jordan. 

Kwa sasa juhudi za kuwatafuta watu 17 waliopotea zinaendelea na kwamba mamlaka pia inaendelea na mchakato wa kuisafirisha miili ya waliokufa hadi Jordan ili kuizika. Kwa kuzingatia viwango vya joto viliyopo eneo hilo kwa sasa mamlaka nchini Saudi Arabia iliwahimiza mahujaji kubeba miamvuli maalum kujikinga dhidi ya jua. VOA

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet