Maj Gen Fatuma awa mwanamke wa kwanza kuongoza Jeshi la Anga
Eric Buyanza
May 2, 2024
Share :
Meja Jenerali Fatuma Ahmed ameandika historia nchini Kenya baada ya kuteuliwa na Rais Ruto kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza Jeshi la Anga la nchi hiyo.
Meja Jenerali Fatuma alijiunga rasmi na Jeshi la Kenya mwaka 1984 na amekuwa mwanamke wa kwanza katika miaka kumi iliyopita kupandishwa cheo kuwa Brigedia na baadae kuwa Meja Jenerali.