pmbet

Majaliwa ataka madereva kutunza siri za mabosi wao

Eric Buyanza

August 21, 2024
Share :

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ameelekeza wadereva wa serikali wanapokuwa na viongozi katika magari, wajitahidi kutunza siri kwa kuwa wanabeba dhamana ya nyaraka za serikali. 

Pia amewataka kutokuingilia na kuchangia maongezi wakati viongozi wakizungumza na watu wengine kwa njia ya simu, hasa wanapokuwa ndani ya gari.
Waziri Mkuu aliagiza hayo jana jijini Arusha wakati akifungua Kongamano la Tatu la Madereva wa Serikali.

"Unakuta kiongozi anazungumza kwa simu akiwa ndani ya gari kisha dereva anaingilia mazungumzo pasipo kujua kiongozi huyo anazungumza na nani, huo ni utovu wa nidhamu, ukosefu wa maadili, uvunjivu wa nidhamu na ni kinyume cha sheria na kanuni za udereva," alisema Waziri Mkuu.
Majaliwa alisema madereva wa serikali wanapaswa kuwa na siri pindi wanapokuwa na viongozi katika magari kwa kuwa wanabeba nyaraka za serikali na suala la siri ni muhimu kwa kuwa siri ni sehemu ya nyaraka hizo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet