pmbet

MAJARIBIO ZAIDI YA 100, MABAO 8: Jinamizi la umaliziaji linavyoitesa Man United

Eric Buyanza

September 21, 2026
Share :

Miamba ya soka nchini Uingereza, Manchester United, imeweka rekodi ya kipekee lakini ya kusikitisha msimu huu, baada ya kuwa klabu ya kwanza katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kufikisha na kuvuka majaribio 100 ya kufunga langoni. Hata hivyo, ufanisi wao mbele ya lango umekuwa wa hovyo, huku wakiambulia mabao 8 pekee hadi sasa.

 

Takwimu zinaonyesha kuwa United imepiga jumla ya mashuti 113 katika michezo yao mitano ya kwanza ya msimu huu wa 2026/2027. Licha ya mashuti hayo yote, kiwango chao cha kubadili nafasi hizo kuwa mabao (conversion rate) kimeshuka mnoo, jambo linalowaweka kwenye wakati mgumu na kuwaacha katika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi.

 

Kati ya mashuti 113 yaliyopigwa, ni mashuti 28 pekee yaliyolenga lango (shots on target). Idadi kubwa ya mashuti imekuwa ikitoka nje au kuzuiwa na mabeki wa timu pinzani.

 

Wachambuzi wa soka wamebainisha kuwa tatizo la Manchester United si uwezo wa kutengeneza nafasi, bali ni ukosefu wa utulivu na umakini kwa washambuliaji wake.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet