Majeneza 150 yateketea kwa moto, mafundi wapagawa
Eric Buyanza
March 19, 2024
Share :
Zaidi ya majeneza 150 ambayo mafundi walikuwa wametengeneza na kusubiria wateja yameteketea kwa moto hadi kuwa majivu huko mjini Karatina nchini Kenya.
Mmoja wa mafundi hao Bw James Njogu, alisema amepoteza majeneza 16 ambayo alikuwa ameweka katika duka lake kusubiri wateja.
“Manne kati ya hayo majeneza 16 tayari yalikuwa yamenunuliwa na kilichokuwa kimebakia ni wateja kuja kuyachukua” alisema Bw Njogu.
TAIFALEO